18 May 2012

CANDY - CHANINI

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.



Studio ya Pamoja Records imeachia single mpya ya yule mwanadada candy ambaye mwezi mmoja uliopita aliachia ngoma yake inayokwenda kwa jina  nimpende milele ikiwa chini ya Most Records.

Leo hii Pamoja Records imeachia single ya mwanadada huyo inayokwenda kwa jina la “Chanini”, candy msanii ambaye licha ya uimbaji pia anakipaji pia cha kucheza miziki  ya aina zote.

Candy ambaye mtaani anajulikana kwa jina la (candy tikisa!! Au candy wa Kujiachia..!) , ambaye amejipatia umaarufu mkubwa pale aliposhiriki mashinbdano ya Kucheza muziki  yaliyokuwa yanajulikana kama “tikisa” ameachana na lebo ya “most Record ” na kupata ofa nyingine kwenye studio za pamoja record jijini dar es salaam, Ambayo tayari amesharekodi single yake hiyo moja inayoitwa “chanini” ambayo tayari imeshaanza kupigwa kwenye vituo mbalimbali vya redio.

Kwanini ameachana na Most Records?
Candy anajibu  kuwa hawakuelewana na management nzima ya Most Records ambapo kwa sasa wapo kwenye mzozo ambao bado haujapatiwa ufumbuzi  Lakini tayari alikuwa amerekodi single moja  pamoja na video ambayo vyote amefanyia Kwenye kampuni hiyo ya most record,  yeye candy ameizuia isionyeshwe kwenye vituo vya television mpaka pale muafaka wao utakapomalizwa.

Candy amewafagilia sana Pamoja Records kuwa wapo sawa na makini sana kwenye kazi na ndiyo maana ameingia mkataba nao na huko atafanya kazi ambayo mashabiki wa muziki watasuuzika na muziki wake.

Details

Atrist: Candy
Track : Chanini
Studio : Pamoja Records
Producer : Nas B.

18 May 2012

Mtangazaji wa kipindi kipya ‘Mboni Show’, Bi. Mboni Masimba kinachotarajiwa kuruka hivi karibuni katika televisheni ya EATV akiongea na waandishi wa habari juu ya kuanza kwa kipindi chake. Pembeni yake ni msimamizi wa kipindi hicho Bw. George Tyson na msimamizi wa vipindi vya EATV. Kipindi hichi cha Mboni Show dhima yake ni kuburudisha, kuelimisha, kufundisha, uonya, uadhibu na kuelekeza jamii ya Watanzania inayokabiliwa na changamoto nyingi katika maisha ya kila siku. Na pia kipindi kinakusudia kuleta mapinduzi makubwa katika muendelezo wa vipindi vya mahojiano.


Meneja wa vipindi kutoka EATV akizungumza katika uzinduzi huo wa kipindi cha Mboni Show kinachotarajiwa kuanza kuruka Mei 31 ndani ya EATV.





Msimamizi wa kipindi cha Mboni Show, Bw. George Tyson akielezea ubora wa kipindi hicho.



Mtangazaji wa Kipindi Kipya Mboni Show, Bi. Mboni Masimba akifanya mahojiano ya waandishi wa habari wa EATV. Mboni Masimba ni binti ambaye ana ndoto nyingi za kutafuta maendeleo, binti anayependa kujituma na anayependa kujifunza kutoka kwa wengine.

Lakini pia anapenda muziki, mitindo na ni mjariamali anayemiliki kampuni yake binafsi iitwayo ‘Chocolate Pincess’ ambayo inaendesha duka la mavazi, vipondozi na viatu vya kike lakini pia ndiyo waandaaji wa kipindi kipya cha luninga ‘The Mboni Show’. Picha zote na www.kajunason.blogspot.com

18 May 2012

TID FT NGWAIR – KIUNO

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

18 May 2012

Wakameruni wapatao zaidi ya 5,000 waishio nchini ujerumani wanatalajia kujimwaga kujirusha na muziki wa dansi wa Ngoma Africa Band huko mjini Stuttgart, Ujerumani siku ya jumamosi 20 Mei 2012, katika sherehe maalum ya nchi yao “Cameroon Challenge” . Kamati ya maandalizi ya jumuhia ya wakameruni nchini Ujerumani imetoa mwaliko kwa bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band almaarufu FFU, kutumbuiza katika sherehe hizo zitakazo fanyika mjini Stuttgart, nchini Ujerumani, ambako zitahudhuriwa na wakameruni 5000 pamoja na wageni wa mataifa mbali mbali.

Mzimu huo wa dansi Ngoma Africa band aka FFU unatarajiwa kutoa burudani ya kuwapandisha mzuka wadau wote watakao jimwaga uwanjani, Ngoma Africa band sasa wanatamba na wimbo mpya “Uhuru wa Habari” sikiliza @ www.ngoma-africa.com

17 May 2012

AT – HARUSI

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

17 May 2012

PATRICK Mutesa Mafisango (32), mchezaji tegemeo wa Simba SC amefariki dunia jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo katika eneo la Keko jirani na Chuo cha VETA jijini Dar es Salaam.

Mafisango alikufa kutokana na ajali iliyotokea wakati gari alilokuwa akiendesha lilipogonga mti ulio pembezoni mwa barabara ya Chang’ombe majira ya saa kumi kasorobo alfajiri. Marehemu alifariki papo hapo.

Kwenye gari aliyokuwamo Mafisango, kulikuwapo na abiria wengine wanne lakini ni Mafisango pekee ndiye aliyefariki dunia.

Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tayari kwa kusafirishwa kwenda kwao Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako atazikwa.

Ingawa alikuwa na uraia wa Rwanda na akiichezea timu ya taifa ya nchi hiyo (Amavubi), Mafisango alikuwa ni mzaliwa na raia wa DRC na uamuzi wa kuzikiwa huko ni wa familia yake.

Msiba wa Mafisango uko katika eneo la Keko Toroli jirani na kituo cha Chang’ombe Maduka Mawili (Njia Panda Sigara).

Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa kesho Ijumaa saa nne asubuhi katika viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es Salaam kabla ya mwili wake kusafirishwa kwenda Kinshasa majira ya saa kumi jioni.

Mafisango alizaliwa Machi 30, 1980 huko Kinshasa Zaire wakati huo na ameacha mke na mtoto mmoja wa kiume, Chris Paul, mwenye umri wa miaka mitano.

Mafisango ameichezea Simba kwa msimu mmoja tu akitokea Azam ya Dar es Salaam lakini kabla ya hapo alichezea pia TP Mazembe ya DRC, APR ya Rwanda na pia aliwahi kuwa nahodha wa Amavubi kwa takribani miaka mitano.

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, Makamu wake, Geofrey Nyange Kaburu na wajumbe wa kamati ya watendaji wameeleza kusikitishwa kwao na msiba huu mkubwa kwa klabu na wamewataka wana Simba wote kuwa watulivu na kumwombea marehemu Mungu amlaze mahali pema peponi.

Uongozi wa Simba unaahidi kuwa utatoa taarifa nyingine zozote muhimu kwa wananchi ili wafahamu kuhusu msiba huu pale itakapotokea.

Imetolewa na:
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari - Simba SC
17/5/2012

Page 12345678910203040...

SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!