Archive | March, 2011

08 March 2011

——–
MSHAMBULIAJI
Thomas Ulimwengu, ameitwa katika timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa. Akizungumza Dar es Salaam, jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF), Boniphace Wambura, alisema Ulimwengu anatarajia kuondoka Machi 11, kwenda Lubumbashi.
————–
Wambura alisema mchezaji huyo atakwenda kufanya majaribio hayo akiwa chini ya wakala wake Damas Ndumbaro, ambaye ni wakala anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA). Alisema licha ya kwenda kufanya majaribio hayo, mchezaji huyo atalazimika kuombewa ruhusa katika timu hiyo ili aweze kujiunga na wachezaji wenzake katika timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23. Alisema timu hiyo itacheza mchezo wake wa awali na Cameroon katika michuano ya kuwania kucheza mashindano ya Olimpiki. Alisema taratibu nyingine kwa ajili ya safari ya mchezaji huyo tayari imekwishakamilika na kusema kwa sasa mchezaji huyo yupo katika maandalizi ya kwenda nchini humo. Ulimwengu atafanya majaribio nchini humo kwa mara ya pili ambapo awali aliwahi kufanya majaribio katika timu ya daraja la kwanza ya Dalkurd.

08 March 2011

-

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.


-
Nyimbo mpya ya Mwana FAUNANIJUA UNANISKIA
_

07 March 2011

MPIGIE kura Msanii Joh Makini kutoka A-City aweze kunyakua tuzo za Kilimanjaro zitakazofanyika hivi karibuni
——————————-
Wimbo bora wa Hip HopKaribu Tena
Tuma J146 kwenda namba 15747
——————————–
Msanii bora wa Hip Hop - JOH MAKINI
Tuma N143 kwenda namba 15747

————————–

07 March 2011

NGULI wa filamu nchini Vicent Kigosi a.k.a Ray ameoenekana kuwa juu katika tasnia hiyo kutokana na filamu yake ya Family Disaster kufanya vizuri sokoni.
————-
Hali hiyo inatokana na uchunguzi uliofanywa na DarTalk katika maduka mbalimbali ya uuzaji wa filamu za kibongo ikaonekana filamu hiyo kuwa juu kimauzo. Kitendo hicho kimefanya kazi hiyo kuonekana na mvuto mkubwa kwa mashabiki wa filamu nchini.

07 March 2011

————–
Baada ya miezi miwili tu kupita tangu Dogo Janja kuamua kuingia shule, Msanii mwingine bwana mdogo matata kwelikweli maarufu kama Young D nae ameamua kurudi skonga.
—————
Young D amesema haya baada ya kushauriana na mama yake kaamua kurudi shule.
—————

07 March 2011

————–
MSANII BORA WA HIP HOP – FID Q
TUMA N139 KWENDA 15747
————-
WIMBO BORA WA HIP HOP – PROPAGANDA
TUMA J168 KWENDA 15747
———
CLICK LINK IFUATAYO KUPIGA KURA KUPITIA TOVUTI

http://www.kilitime.co.tz/awards/2009/nominees_2007.php
—————-

07 March 2011

Msanii anayefahamika kama DIAMOND afanya show kali pale NEW CLUB MAISHA Jupamili katika X-SUNDAY PARTY akisindikizwa na HEMEDI aka PHD.

06 March 2011

———-
MAKOCHA
wa mchezo wa kuogelea waliohitimu mafunzo hivi karibuni, wametakiwa kuyatumia mafunzo waliyopata kwa kuvumbua na kuendeleaza wachezaji chipukizi.
——————-
Hayo yalielezwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Rais wa Chama cha Makocha wa mchezo wa Kuogelea Tanzania (TSCA) Alexander Mwaipasi kwenye hafla fupi ya ufungaji wa kozi hiyo.
——————
Kozi hiyo ambayo ilikuwa ya kimataifa na iliwashirikisha makocha 59, wa ndani na nje ya Tanzania ilifanyika kwenye Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) iliyoko Upanga, Dar es Salaam.
——————-
Hakika hii ni idadi kubwa ya makocha ambayo imejitokeza na kushiriki kozi hiyo, ambayo ilidumu kwa takriban siku nne. Hivyo TSCA inaimani kubwa idadi hiyo ya makocha itatoa chachu ya kuboresha mchezo huo,” alisema.
——————–
Mwaipasi alisema makocha hao wanapaswa kutambua kuwa, siku zote kocha mzuri ni yule ambaye anatumia vema ujuzi wake kwa kusamabaza kwa wengine.
———————
Alisema lakini kocha ambaye anaamua kurundika tu ndani vyeti, ilimradi  aonekane amesoma na ana kiwango cha juu hatimaye huwa ni kuzorotesha ujuzi na kukwamisha mchezo husika.
“Hakuna maana yoyote kwa kocha kujirundikia vyeti vya kila aina ndani, ila kocha bora ni yule anayetumia elimu yake kwa kuendeleza mchezo husika. Ninategemea wengi wa wahitimu walipa kipaumbele suala la kuendeleza mchezo wa kuogelea nchini,” alisema.
——————–
Alisema washiriki wa mafunzo hayo walitoka nchi za Zambia, Uganda na Tanzania, ambayo ilikua na idadi ya zaidi ya makocha 50 kutoka mikoa mbalimbali.

05 March 2011

————-
Wimbo: ACTION- CPWAA ft Ms. Triniti. Dully Sykes & Mangwear.

Nomination:
Video bora ya mwaka: Tuma neno S 129 Kwenda namba 15747
Wimbo bora wa ragga/dancehall:  Tuma neno L 129 kwenda 15747
Kila SMS ni TSH 100 tu! au tuma kura zako ( L 129 na S 129)
——————
Kwa barua pepe kwenda ktma@innovexdc.com
—————–

05 March 2011

“Ruge hata afanyaje,studio ya wasanii ambayo alimuingiza mkenge rais kikwete ni lazima itarudi mikononi mwa wasanii wa tanzania kama ambavyo kikwete alitangaza ndani ya bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania kuwa amewapa wasanii wa tanzania studio pamoja na pango la nyumba ya kuendeshea hiyo studio,kikwete hakusema alimpa ruge,tht wala hicho chama hewa ambacho hakijasajiliwa kisheria na basata kinachoitwa ‘tanzania flava unit’…na ole wao wasanii vibaraka wanaotumiwa na ruge kupitia chama hiki  kukwamisha jitihada zetu,ghadhabu ya kitaa itawashukia na hakika hawataliweza balaa lake…peooooples…poooower!!!” alisema SUGU

Page 8 of 9123456789

SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!