UTENGENEZAJI WA VIDEO MPYA YA MIAKA 50 YA UHURU…!!
17 May 2011

Posted on 17 May 2011

UTENGENEZAJI wa video ya wimbo unaozungumzia miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika umeanza kufanyika leo katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ikiwemo Uwanja wa Taifa, Kituo cha Utamaduni cha Watu wa Urusi na kwingineko.

Wimbo huo umetayarishwa na Marco Chali wa Mj Records na Lamar wa Fish Crab, kazi ya video inafanywa na Adam Juma wa Visual Lab Next Level.

Matengenezo ya mwisho yamefanywa katika studio aliyotoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Kikwete ili iweze kuwasaidia wasanii katika kazi zao.

Baadhi ya wasanii walioshiriki katika wimbo huo ni pamoja na Fid Q, Cassim, Madee, Barnaba, Linah, Mwasiti, Diamond, Jaffarai, TID, Amini, Tundanga, Banana Zorro, KR, Chege, Temba na wengineo.

Ni wasanii 34 wameshiriki kuimba wimbo huo, ambao utaachiwa hewani pamoja na video yake wakati wowote.

PICHA KWA HISANI YA BONGO STAR LINK

Tags , , , , , , , , , , , , , , , , , ,
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!