“BOB RUDALA” KIFAA KIPYA CHA BENDI YA KALUNDE…!!
16 June 2011

Posted on 16 June 2011

Kifaa kipya cha bendi ya Kalunde, Bob Rudala mwishoni mwa wiki alikuwa kivutio katika maonesho ya bendi hiyo, yaliyofanyika ktk kumbi kadhaa jijini Dsm.

Bob Rudala ambaye awali alitamba na bendi ya In Afrika, aliwashika vilivyo mashabiki wa bendi hiyo waliohudhuria maonesho hayo haswa baada ya kuweza kwenda sambamba ktk nyimbo mpya za bendi hiyo za Fungua, Masumbuko na Sisee.

Licha ya kutamba na nyimbo hizo, Kalunde pia iliweza kutumbuiza nyimbo zao za zamani zilizopo katika albamu ya Hilda.

Akizungumzia ujio wa Rudala,Rais wa bendi hiyo Deo Mwanambilimbi alisema “Baada ya kumnasa Bob Rudala katika bendi yetu, hivi sasa tupo katika hatua za mwisho kukamilisha nyimbo nyingine tatu ambazo zitachanganywa na alizokuja nazo Rudala,” alisema Mwanambilimbi.

Habari na darhotwire

Tags , ,
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!