
Posted on 20 June 2011

Kundi la Face 2 Face likiwa jukwaani likonesha umahiri wake wa kutaka kuibuka mshindi kwenye shindano la kumsaka mkali wa msimu wa dhahabu unaoendelea wa serengeti dansi la fiesta 2011, lililofanyika katika ukumbi wa New Maisha Club jijini dar, ambapo watu kibao walijitokeza kulishuhudia shindano hilo ambalo lilikuwa limejawa na msisimko mkubwa.

Kundi la Under Zone wakionyesha umahiri wao wa kucheza mbele ya mashabiki wakati wa kulisaka kundi bora la msimu wa dhahabu unaoendelea.

Kundi la Ice Cream kutoka jijini Tanga likisubiri majibu mara baada ya kuonyesha umahiri wao wa kucheza

Mashabiki wakifutilia kwa makini mchakato wa kulisaka kundi bora la msimu wa dahahbu unaoendelea wa Serengeti dansi la Fiesta 2011 ndani ukumbi wa New Maisha Club, jijini Dar

Majaji wa Serengeti Dance la Fiesta 2011 kutoka kulia ni mtangazaji wa Clouds Fm 88.4 jijini Dar es Salaam Hamis Mandi a.k.a B Dozen, Msami kutoka Tanzania House of Talents pamoja wa muandaaji wa kipindi cha ‘Step Up Player’ cha Clouds Tv, Isakwisha Thomson

Vijana kutoka jijini Dar, kundi la Still Unity wakionyesha manjonjo yao mbele ya mashabiki.

Kundi la Bsix kutoka Zanzibar wakionyesha umahiri wao wa kucheza kwa namna ya kipekee.

Mmoja wa majaji kutoka Clouds TV,Isakwisa Thomson akifafanua jambo.
Picha Zote na John Bukuku