“JINI KABULA” AMEKANUSHA KUFUNIKWA NA WASANII WANAOCHIPUKIA…!!
03 July 2011

Posted on 03 July 2011

Mcheza sinama za Bongo, Mariam Jolwa a.k.a Jini Kabula amekanusha kufunikwa na wasanii wanaochipukia kwenye tasnia hiyo wanaodaiwa kuigiza kuwa usitadi mkubwa kuliko yeye.

Jini Kabula alisema kuwa hayupo kwenye fani hiyo kwa ajili ya kushindana bali anatumia kipaji alichopewa na Mungu kufikisha ujumbe ambao hulenga kuufikisha katika jamii kupitia sehemu ambazo hucheza.

Aliendelea kufunguka kuwa, kilichomtambulisha katika fanii hiyo ni nafasi ya jini ambayo alifanikiwa kuicheza kwa ustadi na watu kuamini kuwa yeye ni jini kitu ambacho anadai hakiwezi kufutika haraka kichwani mwa watu.

“Kwenye tasnia ya filamu nilitambulika kama jini na hilo ndilo jina lililonitoa hivyo hakuna wa kunishinda ninajiamini na ninauwezo mkubwa wa kucheza kila sehemu ninayopewa kufanya hivyo, sipo kimashindano bali najivunia kipaji changu” alisema Jini Kabula.

Habari / Picha na GPL

Tags ,
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!