LUDACRIS ALONGA NA WANAHABARI, AHAIDI MAKAMUZI YA HATARI KWENYE TAMASHA LA SERENGETI FIESTA JUMAMOSI…!!
29 July 2011

Posted on 29 July 2011

Mwanamuziki Ludacris kutoka nchini Marekani akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika mapema asubuhi kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dare es salaam, Ludacris alikuwa akizungumzia onyesho lake atakalolifanya kesho, katika tamasha la Mwendelezo wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta, linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye viwabja vya Leaders Club jijini Dar es salaam, katika picha kulia ni Mkurugenzi wa radio Clouds Ruge Mutahaba. Ludacris amesema anazo albam saba hivyo katika albam hizo anatarajia kutoa burudani ya kutosha ili kukonga mioyo ya mashabiki wa wa muziki wake nchini Tanzania



Mwanamuziki Ludacris wa pili kutoka kulia akiwa katika mkutano huo kulia ni Ruge Mutahaba mkurugenzi Clouds kushoto ni Caroline Ndungu, aliyekuwa mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweriers na Meneja wa bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo.


Meneja wa bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo akizungamza katika mkutano wa waandishi wa habari wakati alipozunguzia tamasha la Serengeti Fiesta, linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye viwanja vya Leaders Club, katikati ni Mwanamuziki Ludacris na mwisho ni Mkurugenzi wa Clouds Ruge Mutahaba.


Habari / Picha na John Bukuku

Tags , ,
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!