JACK KUJA NA IZZO B, QUICK ROCKER KATIKA FILAMU YA TIME AFTER TIME..!!
17 September 2011

Posted on 17 September 2011

MWANADADA Jacqline Wolper anayetisha katika Filamu Bongo anakuja na wasanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo Fleva, Izzo B na mwenzake Quick Rocker katika filamu yake mpya inayjulikana kwa jina la Time After time wasanii hawa ambao wamejulikana kupitia muziki wanazidi kujipanua kupitia filamu na kuwa na kipaji zaidi kimoja.

Akiongea na Filamu Central Jack anasema kuwa kwa sasa ana kazi nyingi sana ambazo yeye ni mtayrishaji kwa hiyo pamoja na kutafuta ubora wa kazi zake pia anatumia muda huo huo kuangalia wasanii ambao anaamini kuwa wanaweza kuigiza ikiwa pamoja na muonekana katika uigizaji na kuwapa nafasi ili kuonyesha vipaji vyao.

“Nimemaliza filamu nyingine hivi karibuni ndiyo nimetoka sehemu ambazo nilitumia kurekodi, filamu yangu ya Time after time nimeleta wasanii wenye fani yao tofauti na kuigiza lakini wanaigiza tena kwa kiwango kikubwana nawakutanisha wasanii wanaofanya vizuri katika muziki wa bongo fleva Quick Rocker na Izzo B,”anasema Jack.

Mbali ya wasanii hao katika filamu ya Time After time pia unakutana wasanii wengine wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu kwa sasa na toka kitambo kama vile Irene Uwoya, Rachel Haule pamoja na wasanii wengine wakali.

Habari na FilamuCentral

Tags , , ,
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

One Response

  1. jema ngowi says:

    jitahidi wolper coz wewe ni mkali na unaweza .nakupa big up ile mbaya


LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!