Posted on 29 December 2011
MSANII wa muziki wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’, amekanusha vikali habari zilizotolewa na aliyekuwa mwakilishi wa miss Swahili Rehema Fabian, kuwa aliwahi kutembea naye.
Fabian alizungumza na DarTalk, hivi karibuni na kusema kuwa Diamond hana mvuto wa mapenzi na kama alitembea naye sasa basi na aendelea na hao anaowachezea.
Diamond sasa ameamua kufunguka baada ya kupata taarifa hizo na kusema kuwa hakuwahi kutembea na mrembo huyo kwani anatafuta umaarufu kupitia jina lake.
“Nilisoma habari ambayo alikuwa ananielezea mimi hivyo sikupenda alivyosema, lakini naweza kusema kama ananitaka ni heri awe muwazi kuliko kuzungumza maneno ambayo hayana maana,” alisema.
Hata hivyo alisema kuwa kwa sasa yupo busy na mambo yake na endapo anataka kutembea naye kwake hana nafasi huku akimpa makavu kuwa hana hadhi ya kuwa na yeye.
Dah tatizo wasanii wengi wa kibongo wakisha kuwa masuper star wanajiona wao ndo wao.hawajatulia kabisa