Posted on 02 January 2012
MSANII wa muziki wa bongo Fleva Mwana FA, ameuambia mtandao wa burudani wa DarTalk kuwa fani hiyo kwa mwaka uliopita imepiga hatua kubwa na kuwapa wasanii wengi mafanikio.
Alisema kuwa mafanikio waliyopata wasanii hao, yote yametokana na upokeaji mzuri wa kazi zao kutoka kwa Watanzania ambao wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika kila kazi wanazotoa.
Msanii huyo kwa sasa anatamba na track yake ya ‘Yalaiti’, aliyoitoa mwishoni mwa mwaka jana huku akishirikiana na mwanadada Linah.
“Unajua kazi ya sanaa inabadilika kila mwaka hivyo naweza kusema nyota wengi msimu uliopita wameweza kufanya vizuri lakini wapo wengine ambao hali ilikuwa ni tete kwao na hao siwezi kuwasemea kwani kila mtu anamipango yake katika game,” alisema.
FA alisema kuwa mwaka huu anajipaga vyema katika kuleta mapinduzi ya fani hiyo ambayo inazidi kukua siku hadi siku huku vijana wengi wakijikata katika kuimba pekee.
big up bro u a duing great lakini mna mpango gani na bro wenu GK??? au ndo mnataka apotee kabisa…… tell also Ay and you should both think about that.