
Posted on 05 January 2012
MSANII wa muziki wa Regge bongo, anayefanya vizuri na Band ya ‘Afrikabisa band’, Jikhoman, amesema anatarajia kutoa ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina ‘Bongo Ragga Mussin’.
Akizungumza na DarTalk, msanii huyo alisema baada ya kuachia wimbo huo atakuwa katika harakati za kuachia albamu yake yenye nyimbo 10.
Jikhoman alizitaja baadhi ya nyimbo hizo kuwa ni ‘Bongo Ragga Mussin’, ‘Afro Regge’, ‘Moyo Unadunda’ na nyingine nyingi ambazo zote zimeandaliwa katika kiwango cha kimataifa.
“Natarajia kutoa wimbo huo pia baada ya kutoka kwa kazi hiyo nitakuwa katika maandalizi ya kuachia albamu yangu, ambayo imeandaliwa katika kiwango cha kimataifa,” alisema.
Jikhoman pia aliongeza kuwa anawasihi mashabiki wake kuisubili albamu hiyo kwani kazi zake huwa anazifanya kimataifa na kwa kufuata tamaduni za Kiafrika.