FROLA MVUNGI AJIWEKA KWA DEREVA WA MABASI YA MIKOANI…!!
28 January 2012

Posted on 28 January 2012

BAADA ya kuachana na H-Baba, msanii Frola Mvungi, amesema sasa amejiweka kimapenzi kwa dereva wa mabasi yaendayo mikoani kwa kile alichodai kuwa ni fundi katika mapenzi kuliko wote aliowahi kutembea nao.

Akizungumza na mtandao wa burudani wa DarTalk, nyota huyo alisema mpenzi wake huyo mpya alimpata katika ukumbi mmoja wa starehe uliopo Sinza.

Alisema kuwa baada ya kukutana na mwanaume huyo hakusita kuzungumza naye, na baada ya hapo walipanga kukutana tena siku nyingine na hapo ndipo walipoamua kuanzisha mahusiano ya kimapenzi kwani walizungumza na muda mrefu na kufikia uamuzi huo mzito.

“Mapenzi si pesa wala si ustaa hivyo nimeamua kumpenda mtu ambaye hata hajulikana kwani naamini hata baadhi ya wasanii waliozoea kuchukuliana wanaume hawawezi kumpata kwa sababu kila siku yuko bize na kazi zake,” alisema.

Na Laurent Samatta

Tags ,
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

One Response

  1. masesa lenadi says:

    Mimi ni mdau mpya ktk mtandao naomba masela kwa moyo mmoja nipo pande za kahama mambo mengi napenda kufahamu kutoka kwenu nipigeni tafu napendelea hasa music & filamu hasa za majuuuu


LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!