
Posted on 09 February 2012
BAADA ya kudaiwa kuwa anatumia dawa za kichina za kuongeza makalio, msanii wa filamu bongo, Zena Muhamed ‘Shilole‘, amekanusha vikali ishu hiyo na kudai kuwa haina ukweli wowote ndani yake.
Msanii huyo aliwaambia rafiki zake wa karibu kuwa anazisikia dawa hizo lakini makalio yake ni ya kuzaliwa nayo na tangu alipokuwa mtoto alikuwa na makalio hayo.
Wakati Shilole, anazungumza na rafiki zake kuhusu ishu hiyo, mwandishi wa DarTalk, alikuwa karibu ambapo, alimuuliza msanii huyo ni kwanini katika nyimbo zake anaonesha makalio yake huku akiwa anayachezesha?. Alijibu kuwa hiyo huo ni ubunifu wake kwani watanzania wengi wanapenda makalio makubwa hivyo anaamini kuna baadhi ya watu wanapenda kazi zake ili waone anavyokatika.
Alisema haoni kama ni kitu cha kushangaza sana kwababu wapo baadhi ya wasanii ambao ndiyo mabingwa wa kutumia dawa za kichina za kuongeza makalio pamoja na matiti.
Na Laurent Samatta