
Posted on 17 February 2012
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Z-anto, inasemekana kurudi katika kundi la zamani la ‘Tip Top Conection’, lenye maskani yake Masenze Dar Es Salaam kwea ajili mazungumzo ya kama anaweza kufanya nao kazi.
Msanii huyo alikuwa ni mmoja ya nyota wa kundi hilo lakini aliamua kujitoa kutokana na sababu mbalimbali za kimaslahi.
Habari zilizopatikana kwa mmoja wa wasanii wa kundi ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema, wenda wakachukua wasanii wengi lakini wapo baadhi ambao wana uwezo ndiyo watakaochukuliwa.
Alisema kuwa Z, ni moja ya nyota ambao wana uwezo mkubwa kimziki lakini hawajui kama anafikiria kurudi tip top.
“Hatujui lakini mazungumzo yapo hivyo tunaamini anaweza kurudi kwa sababu sisi wote ni wasanii hivyo hatuna budi kusema kama anaweza kuja au laa na majibu yote anayo yeye,” alisema msanii.
Hata hivyo DarTalk, ilipojalibu kumfuta Z-anto, hakuweza kupatikana kwenye simu yake ya mkononi.
Na Laurent Samatta