GABRIEL MOLLEL NI MBUNIFU ANAYETAMBA NA MAVAZI YA KIMASAI…!!
30 March 2012

Posted on 30 March 2012

MBUNIFU mahiri wa mavazi ya Kimasai nchini Gabriel Mollel, amesema kuwa ataendelea kuzinadi nguo za kabila hilo kwani ndizo nilizompa umaarufu mkubwa hadi kufika hapo alipo sasa pamoja kufanya maonesho makubwa ndani ya nje Afrika.

Akizungumza na DarTalk, mbunifu huyo alisema kuwa amekuwa akifanya vizuri kupitia mavazi ya kimasai na hadi kupata mialiko ya nje ya nchi kutokana na ubora wa staili yake ambayo wabunifu wengi hawana.

Alisema kuwa nwaka 2011 alichanguliwa kwenda kushiriki katika mashindano hayo ya mavazi nchini Angola na mavazi yake yalionekana kufanya vizuri kwani aina kubwa ya nguo zake ni za kimasai.

Aliongeza onesho hili lilihudhuliwa na wabunifu zaidi 40 kutoka nchi mbalimbali Afrika lakini kutokana na ubora wa nguo zake watu walizipenda kwa kiasi kikubwa.

“Naweza kusema kwamba mimi bado ni chipukizi katika tasnia hii ya ubunifu lakini hadi hapo nilipofika watu wameweza kunikubali kwa kiasi kikubwa sana,” alisema.

Mbali na hayo pia aliongeza kuwa amejiwekea malengo mengi ndani ya kichwa chake kwani anahitaji kufika mbali zaidi katika fani ambayo tayari imeshawatoa watu wengi.

Na Laurent Samatta

Tags
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!