
Posted on 11 April 2012
WASANII wanaounda kundi la ‘Together Group’, Salma Jabu ‘Nisha’ na Frola Mvungi, wamedai kuwa wameshaachia ngoma yao inayokwenda kwa jina la ‘Sinaga’ ikiwa katika video na Audio.
Wakizungumza na mwandishi wetu nyota hao wanaotesa ndani ya bongo movie walidai kuwa tayari wimbo yao imeanza kupigwa kwenye vituo mbalimbali vya redio na televisheni.
Frola Mvungi alisema kuwa baada ya kazi hiyo wakutakuwa katika maandalzii mengine mengi ambapo wimbo wao wa pili watakaokwenda kuufanyia Kenya.
“Wimbo wetu wa pili tunaenda kuufanyia Kenya pamoja na msanii wa huko, hivyo tunasubili ili tuone kazi itakuwaje na baada ya hapo tutajua mipango inakuwaje,” walisema.
Hata hivyo msanii huyo aliongeza kuwa mipango na malengo yao katika tasnia ya mziki ni kuonesha uwezo wao kwani wamekuja kuwafunika wale wanaojiona wanaweza.