Posted on 13 April 2012
MSANII wa muziki bongo anayefanya kazi zake Nairobi Kenya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amedai kuwa anatamani kurudi nyuma na kuendelea na kazi yake ya awali ya utangazaji na u-Dj kwa madai kuwa bado anauwezo mkubwa na kazi hizo.
Akiongea na mwandishi wetu kwa njia ya mtandao, Ray C, anaamini fani hiyo ya utangazaji bado anaiweza hivyo anafikiria kurejea bongo na kuendelea na kazi hiyo katika kituo atakachoamua kuomba kufanya kazi.
Ray C, awali kabla hajaanza muziki alikuwa akitangazaji pia Dj, katika kituo cha redio Clouds FM akiwa na kipindi chake cha miziki ya Hip Hop, R&B na Taarab ambapo alichokipa jina la “Dr Beat”.
“Kuna watu hawajui kama mimi niliwahi kufanya kazi hii, lakini kazi yangu ya kwanza kufanya ilikuwa ndiyo hii tena baada ya kumaliza elimu yangu ya Sekondari tu,” alisema.
Hata hivyo anadai kuwa anapenda kujifunza zaidi U-Dj, kwani fani hiyo anayeipenda kuliko kitu kingine chochote ingawa si zaidi ya muziki anaofanya.
Na Laurent Samatta
Ray c, hata hivyo unafaa ilatatizo lako hurithiki ila mungu kama amekupangia kupata utapata tu nafatiliaga sana taarifa zako, Nairobi ulisema umepata kazi ya uwakala wa vinywaji naona umeona hailipi Rudi bongo Dada,
RAY C,HAPO MAHALI ULPO SASA TAZAMA UPEPO WAKO UNAELEKEA WAPI KWA SASA KAMA KWENYE MUZKI UNAONA UMEPOTEA YA BD URUDI KWENYE KIPAJI CHAKO CHAUTANGAZAJI KWA SABABU UWEZO WA SAUTI NZURI NDO INAKUFANYA USHNDWE KUJUWA NKIPI CHA KUEKEZA KATKA LIFE LAKO LA UZEENI ,ME ANOLD NAKUSHAURI URUD KWENYE UTANGAZAJI MZKI UMEKUSHNDA DADA YANGU!!!!!!!!!MWSHO NAKUPA BG UP HAD KUFKA HAPO ULPO SASA ……….ILA MSHUKURU MUNGU ALYEKUPA UZURI ,SAUTI MURUWA TAMBUWA WAPO WA2 WANATAMAN WAWE KAMA WEWE ILA NDO IVO UMEPEWA WEWE TUMIA KIPAJI CHAKO KWA UANGALIFU!!!!!!!!!!!!
eeeeeeeeh!kaz ipo ila 2nakukarbsh kweny hii tasnia ya habari na mawaslano kwan hata hvyo umrth ur c* mheshmwa Betty mkwasa