MISS UTALII KINONDONI 2012 KUFANYIKA CLUB SUN CIRRO…!!
16 April 2012

Posted on 16 April 2012

Shindano la kumpata Miss Utalii Kinondoni 2011/2012 ngazi ya wilaya limepangwa kufanyika katika ukumbi wa kisasa na Club ya kimataifa ya Sun Cirro, iliyoko Shekilango Sinza. Shindano hilo limepangwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 25 Mei 2012 na kushirikisha mabinti 25 kutoka katika majimbo yote ya wilaya ya Kinondoni.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mkurugenzi wa Miss Tourism Tanzania Organisation wilaya ya Kinondoni Pius Yalula, ambao ndio waratibu na waandaaji wa shindano hilo, washiriki wote wanatarajia kuanza kambi ya mazoezi katika ukumbi huo siku ya Jumatatu Mei 1,2012. Miss Utalii Kinondoni 2010/2011, Sophia Dioa ambaye pia ni Miss Utalii Dar es Salaam 2010/2011 na Miss Utalii Tanzania 2010/2011.

Piusi Yalula alibainisha kuwa ni mpango mkakati wa Miss Tourism Tanzania organisation mwaka huu, wa kuwafuata watanzania hususani vijana katika maeneo yao ya burudani, ili kuwahamasisha juu ya utalii wa ndani.

“Ndio maana fainali za mwaka za Miss Utalii Kinondoni, tumeamua kuzifanyia katika Club ya Sun cirro, ambako tunaamini kuwa vijana na watu wa rika mbalimbali wanapenda kwenda katika kumbi na club za aina hiyo kwa ajili ya burudani na mapumziko ya wikendi.” alisema

Tags
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

One Response

  1. Priiscilaa says:

    Kwame, Mabomba ya nuwa haya na maji kwa muda mwingi, hivyo hata ya kikpsuaa sana sana yatatoa hewa. Hayo ni madimbwi ya mvua lakin vile vile maji yanayotoka majumbani, kumbuka kufua ni nje na maji yanamwagwa barabarani, maji ya kuoshea vyombo, maji ya kuoshea mchicha na samaki, maji ya kupigia deki na lisiti ni ndefu. Kwa anony wa kwanza, sikuzote napinga hili wazo la kuoganzizi watu kusafisha bila kuwa na miundombini bora. Kodi wanazolipa zinatakiwa kutengeneza barabara na mitaro halafu ndio wahamasishwe kuweka safi sehemu hizo. Kwa hali ilivyo sasa hawawezi kuondoa madimbwi hayo maana maji hayana pakwenda.


LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!