AUDIO TRACK: CANDY CALIFORNIA – NIMPENDE MILELE
30 April 2012

Posted on 30 April 2012

Hellen David (Candy California) ambaye alikuwa miongoni kwa washiriki katika kinyang`anyiro cha kumsaka mshindi wa “Tikisa 2011” na kutolewa katika hatua za mwisho za shindano lile, ameachia Track yake mpya inayoitwa “Nimpende Milele” chini ya kampuni ya  Most Record & Production ya jijini dar  es salaam. Hellen au kwa jina la kisanii anaitwa “Candy California” ni msanii ambaye anavipaji vingi, licha ya uwezo wake mkubwa wa kucheza muziki wa kila aina pia ana uwezo mkubwa sana wa kuimba. Most Record & Production waliona kipaji chake ndipo hawakusita kumpa ofa ya kurekodi nyimbo pamoja na video.

Baada ya ofa hii aliyopewa na Most  Record & Production, “Candy California” amepata ofa nyingine ya kurekodi nchini Afrika ya Kusini mapema mwezi Juni 2012, ataweka wazi pale mipango yote.

Picha za chini zinaonyesha shooting ya video ya wimbo “Nimpende Milele” ni video ambayo inayoshutiwa na kusimamiwa na Most Production.









Tags
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

One Response

  1. mabulaabe@yahoo.com says:

    da umetisha wangu uko juu


LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!