Posted on 12 May 2012
MWANANADADA tishio katika kupamba video za wanamuziki mbalimbali nchini Agnes Gerald maarufu kama Agnes Masogange ameweka wazi kuchukizwa na tabia ya mastaa wa kike wa bongo muvie kuwadharau wasichana ‘wanaouza sura’ (Video Vixen). Baadhi ya video ni pamoja na ‘Masogange’ ya Belle9, ‘Gube gube’ ya Barnaba na nyingine nyingi.
Mwanadada huyo mwenye umbo la utata, ambaye kuzitendea haki fedha anazolipwa kwa ‘kuuza sura’ alisema kwamba tabia hiyo iliyokithiri imekuwa ikonekana mara nyingi wanapokutana katika mikusanyiko mbalimbali ikiwemo kwenye kumbi za starehe ambapo mastaa wa bongo movie huwaona video Queens hao kuwa si lolote.
“Nawashangaa sana na hizi tabia zao kwani kazi ni kazi tu kama ilivyokwao katika kuigiza, kikubwa ni kila mtu anakula kwa jasho lake…nashangaa wanavyotunyanyapaa tunapokutana klabu,” alisema.
Nt fair jamani
Ningependa kuwashauri kitu kimoja coz ninyi wote ni celebrities wetu then ni kioo cha chetu,tukiwa kama jamii tunajifunza mengi kutoka kwenu si tu kutoka katika kazi zenu bali mpaka katika maisha yenu ya kila,hivyo mnapaswa kuwa makini na mnayoyafanya kwa kufikiria mara mbili jamii inayowatazama itawachukuliaje.Tafadhilini acheni hizo tabia na muwe kitu kimoja kwani hizo zote ni kazi na hakuna wa kumdharau mwenzake kutokana na anachokifanya kwani hiyo ni katika kuelemisha jamii na kujipatia kipato,ingekuwaje kama mngekuwa wahalifu?kuweni makini na achaneni na hizo tabia
ee bwana huyo mtoto masogange noma mbona ananibamba yaani hoi
Dada yangu wewe jaribu kushow luv kwa wasanii wote,msanii ambaye atakua anajitambua basi atarespond luv yako na mtaenda sawa muda wote na yule ambaye atakua anjifanya kukupotezea achana nae coz atakua hajitambui na isitoshe Dada ze2 nyinyi mmekua na udhaifu fulani hasa ukihisi mwenzio ana mvuto kuliko wewe basi inakua ngumu kumpa support.Ni hayo 2 Dada yangu, nakupongeza kwa kazi zako nzuri. Keep it up!!………….
wanakuonea wivu ww ni waukwel ikiwezekana na ww anza kuigiza uzid kuwakimbiza
Dada utavuna utakacho kipanda!Am johnson from Arusha -Booga.