
Posted on 17 May 2012
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi (kushoto) akiongea mchana huu kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Southen Sun, Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Washiriki wa Big Brother Afrika (Julio na Hilda walio katikati) na Waandishi wa Habari. Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Furaha Samalu.

Washiriki wa Big Brother Afrika 2012, Julio na Hilda.

Julio Batalia akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mchana huu kuhusu ushiriki wake katika jumba lile la Big Brother.

Hilda Reiffenstein akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mchana huu kuhusu ushiriki wake katika jumba lile la Big Brother.

Mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Kajuna akiongea na aliyekuwa Mshiriki wa Big Brother Stargame 2012, Hilda Reiffenstein.

Hilda Reiffenstein akiendelea kujibu maswali huku pembeni yake ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Furaha Samalu.

Julio Batalia akijibu maswali huku pembeni yake yupo Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi.

Photo Credit: KajunaSon