Posted on 20 May 2012
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Etisalat, Ahmed Mokhles akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kampuni yao kudhamini shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search, kulia kwake ni mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Productions, Rita Poulsen.
Shindano la BSS mwaka huu litajulikana kama ‘Epiq Bongo Star Search 2012’ ambapo mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 50, pamoja na zawadi nyingine kutoka Zantel, sambamba na mkataba wa kurekodi ili aweze kuendeleza kipaji chake baada ya shindano hilo. Aidha, mchakato wa mwaka huu utakaoanza mwezi June, utawahusisha washiriki kutoka mikoa nane tofauti ikiwemo Lindi Zanzibar , Mbeya, Mwanza, Arusha, Tanga, Dodoma na Dar es Salaam.
bongo star search ya dar inafanyika lini na ukitaka kujiunga unafanyaje?