
Posted on 01 June 2012
ZAIDI ya waigizaji 20 wakali inchini, wameshiriki kuigiza kwenye filamu mpya ya “Bijampola”, iliyoandaliwa na kampuni ya Kinkwin Production. Muongozaji wa filamu hiyo, Marushu Innocent, ameeleza kuwa filamu hiyo yenye maudhui ya kishirikina, mikasa ya mapenzi, na visa vingi ina mafundisho makubu kwenye jamii, anaeleza kuwa filamu hii ni kati ya filamu chache nchini zilizohusishwa waigizaji wengi wenye vipaji, na kikubwa zaidi ni kumuona bamboo ndani ya serious movie.
Filamu imegusa baadhi ya matukio ya kweli yanayotokea kwenye jamii yetu, sisi kama wasanii tunajaribu kugusa kila Nyanja katika kuelimisha jamii yetu hasa katika kizazi hiki ambacho kinaelekea kubaya kwa kukosa maadili, hivyo ni jukumu letu kuilemisha jamii. ni filamu nzuri yenye maadili inayofaa kutazamwa na kila rika alisema, Mohamed Fungafunga (Jengua).
Filamu hii inasambazwa na kampuni ya Kinkwin yenye maskani yake mitaa ya Kimara Korogwe.