NGOMA AFRICA BAND KUVAMIA AFRO-RUHR FESTIVAL, UJERUMANI – JUNI 30…!!
24 June 2012

Posted on 24 June 2012

Kikosi kazi cha Ngoma Africa Band aka FFU yenye makao yake kule Ujerumani,wanategemewa kukwea jukwaa la Afro-Ruhr Festival, siku ya jumamosi 30 Juni 2012 mjini Dortmund, Ujerumani.

Bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya inayoongozwa na mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja wa FFU, itapeleka mzimu wake wote wa dansi katika onyesho hilo kubwa la aina yake,washabiki wa muziki katika onyesho hilo wanakumbana “Jino kwa Jino” na makombora ya muziki wa Ngoma Africa band aka FFU, bendi hiyo kwa sasa inatamba nyimbo zake za “Supu ya Mawe” ,“Uhuru wa Habari” na “Bongo Tambarare” ambazo ipo katika CD ya “BONGO TAMBARARE” pia zinasikika katika kambi yao FFU at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com

Tags ,
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!