Posted on 01 July 2012
BAADA ya Irene Uwoya, kumzungumzia shiti mpenzi wake wa zamani H-Baba, mpenzi wa sasa wa msanii huyo Frola Mvungi, ameamua kuchukua jukumu hilo la kumjia juu Uwoya kwa kudai kuwa hana lolote zaidi ya kutaka kujirudi mpya.
Uwoya alikaliliwa kwenye kipindi kimoja cha Clouds FM akidai kuwa H-baba hajui mapenzi, na hana lolote linaloweza kumuumiza baada ya kuachana.
Hata hivyo kauli hiyo ya kumdhalilisha H-Baba, ilivunjwa ukimya na Mvungi ambapo naye amemchana bila aibu kwa kusema kuwa anachokitafuta sasa ni bifu ambalo kwa upande wao hawana muda naye.
“Uwoya anatafuta bifu ambalo mimi na mpenzi wangu H, hatuna muda naye kwa sababu ni mpuuzi na hana lolote zaidi kuzoea kutembea na wanaume za watu,” alisema Mvungi kwa ukali.
Hata hivyo alidai kuwa maneno anayoendelea kuyatoa Uwoya yana malengo mabaya katika mapenzi yao kwani
anampenda sana H, na hata akiendelea kuzungumzia hivyo kwake yatakuwa hayana maana yoyote.
Hata hivyo mtandao huo ulipomuuliza kuwa bifu hilo linaweza kuisha au litaendelea, alijibu kuwa haliwezi kuisha hadi pale Uwoya atakapoomba msamaha mbele yao.
Mvungi alienda mbali sana na kudai kuwa Uwoya ameshamaliza wanaume hapa na mikoani hivyo anachokitafuta ni umaarufu na wanaume ambao tayari wameshamuona kama maharangwe ya Mbeya.
Hata hivyo Uwoya alipopigiwa simu na muandishi wa habari hizi, alipokea na hakuna aalichojibu zaidi ya kusema kuwa hana muda kurudiana na H- baba kwani hajui mapenzi.
Na Laurent Samatta
wabongo wacheni utumbo
Napenda Kuwashauri Hawa Wasanii Wetu Wa Bongo Kuwa Ugomvi Huna Fd Yyt Kwhy Wanatakiwa Kuangalia Msh Sy Tn Mambo Ya Ugmv