
Posted on 02 July 2012
MSANII anayetesa ndani ya bongo fleva kwa sasa Zena Muhamed ‘Shilole’, ameweka wazi kuwa hawezi kupiga shoo kwa dau ambalo ni chini mil 3.
Kauli ya msanii hiyo anatesa na nyimbo zake kama “Dume dada”, “Nyumba za kupaga”, imekuja mara baada ya DarTalk nafanya naye mahojiano yalitaka kujua anamipango gani ya kuboresha shoo zake.
“Mimi ni msanii mkubwa na ambaye anadhani kuwa nafanya shoo kwa dau dogo imekula kwake anayetaka kunichukua lazima ajipange,” alidai.
Hata hivyo Shilole aliongeza kuwa mwaka huu amepanga kufanya mziki wake kimataifa kwani anaamini anawapenzi wengi nje ya nchi ambao wanapenda sana aina ya mziki anaofanya.