
Posted on 04 July 2012
MSANII na mtunzi wa filamu pamoja na vitabu Tanzania Aunty Fifii, ameuambia mtandao wa DarTalk kuwa baada ya kukamilisha uandishi wa kitabu chake kipya sasa anawasubuli Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), ili wamalizie kukipitia na baada ya hapo kitapelekwa sokoni.
Hata hivyo alisema kuwa anahitaji kukiuza kitabu chake nje ya Bara la Afrika kwani sasa anazungumza na wadau mbalimbali ili aweze kukifanya kiwe na lugha ya kiingereza kwa ajili ya wasomaji wake wa nje.
“Mimi kwa upande wangu nimekamilisha kila kitu hivyo ninaowasubuli kwa sasa ni BAKIKA, ambao nao hata hivyo wanamalizia kukihariri ili kiweze kwenda sokoni,” aliongeza.
Kitabu kimepewa jina la ‘Migororo ya Ndoa na Suluhisho’ , kikiwa na maana kuwa kimechambua migororo yote inayotokea ndani ya ndoa na kuzipatia majibu, huku vijana nao wakiwa wameelezwa namna au njia ya kupata mke bora.