
Posted on 04 July 2012
Mkali wa nymbo miduara ambazo hupendwa sana na mashabiki, Ally Ramadhani “AT”, ameuambia mtandao wa DarTalk kuwa anatarajia kuipeleka videoni ngoma yake ya ‘Bi Harusi’, ili kuwaonesha mashabiki wake picha halisi ya ngoma hiyo.
Msanii huyo mzaliwa wa visiwani Zanzibar ambaye kwa sasa amehamia jijini Dar Es Salaam, alidai kuwa kuipeleka ngoma hiyo videoni kunatamfanya azidi kujiongezea mashabiki wengi watakaoikubali ngoma hiyo.
“Kwa sasa nipo katika harakati hiyo ya kuimalizia kwani kila kitu kinaenda vizuri na mashabiki wangu watarajia kuona ngoma hiyo ambayo ipo katika kiwango kikubwa na kizuri,” alisema AT.