
Posted on 06 July 2012
MSANII wa muziki anayetesa bongo hasa kutokana na sauti yake, Ben Pol, amesema malengo yake kwa sasa ni kuwatoa wasanii chupukizi kwani anaamini kwa kufanya hivyo anataweza kuinua vipaji lukuki.
Kauli ya msanii huyo imekuja mara badaa ya kukutana na mwandishi wetu ambapo alitaka kujua nini mchango wake kwa wasanii ambao wanatafuta kutoka na hawana msaada wowote kutoka kwa wasanii wakubwa kama yenye.
Ambapo alisema mipango ipo na tayari ana wasanii wengi ambao wapo chini yake hivyo anaamini mwaka huu atakuwa amewatoa nyota kibao .
“Mimi nilikuwa chupukizi hivyo najua namna wasanii wanavyosota mtaani, kwa upande wangu nahitaji kuweka historia ndani ya nchi hii kwani wapo wasanii wengi ambao wana uwezo lakini hawatoi mchango kwa chipukizi.” alisema Ben.