“KIONGOZI KAOLE ALINIOMBA RUSHWA YA NGONO” – RAYUU…
06 July 2012

Posted on 06 July 2012

MSANII mrembo ndani ya tasnia ya bongo muvi, Alice Baganzi ‘Rayuu’, amefunguka na kudai kuwa kuna kiongozi wa juu wa kundi la Kaole ‘jina tunalo’, aliwahi kumuomba rushwa ya ngono tena kipindi hicho alikuwa hajavunja hata ungo.

Kitendo hicho kilimfanya ajisikie mpweke kwani hadi wazazi wake walimtaka kujitoa katika kundi hilo ili tu kunusuru maisha yake kuwa matatani.

Wakati akizungumza na mwandishi wa DarTalk, Rayuu alionekana kuumia sana kwani kiongozi huyo hakuwa na haya kutokana na umri wake kuwa mkubwa na yenye alikuwa kama mtoto wake.



Rayuu katika pozi

“Yani nikikumbuka ishu hiyo huwa naumia sana kwa sababu nilikuwa ni mdogo sana, na hadi wazazi waliamua kuambia niacheni na tasnia hiyo,” alidai.

Rayuu hata hivyo aliongeza kuwa kiongozi huyo nia yake ilikuwa kutembea ili ampe nafasi kwenye tamthilia zao ambazo zilikuwa zinafanya vizuri miaka hiyo.

“Lengo lake lilikuwa afanye mapenzi na mimi ili anipe nafasi kwenye tamthilia, na sikuwa tayari niliamua kuwambia wazazi wangu ambapo nao walikuja juu ingawa waliamua niachene na kundi hilo,” aliongeza.

Tags
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

2 Comments

  1. papaa master says:

    siungempa kwan ww unajiona una kitu gan kipya au kwasababu una vipaja vyembamba.

  2. Ashley Ntagomora says:

    Unatafuta Kuvuma. Niwangapi Wamekuchungulia Hujafunguka?. Hivi Siyo Vitu Vya Maadili Kuweka Kwenye Media.


LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!