
Posted on 08 July 2012
KIJANA anayetesa kwenye muziki wa bongo fleva Rich Mavoko, amesema kuwa yupo mbioni kuachia video za ngoma zake mbili ‘Foll Me’ na ‘Merry Me, ambapo zote zitakuwa katika kiwango cha juu ili ziweze kufanya vizuri sokoni.
Ngoma hizo zinafanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya redio na mpango wa kutoa video anaamini utakuwa ni bora zaidi kwani hata mashabiki wa kazi hizo wataweza kuata burudani zaidi.
“Nipo kwenye mchakatow a kutoa video hizo na ngoma ambayo itaanza ni ‘Merry Me’, ambayo watu wengi wamekuwa wakiitaka sana pia baada ya wiki mbili ‘Follow Me’ nayo itakuwa imekamilika,” alisema.