“NYIMBO ZA WASANII WA MIKOANI HAZIPIGWI KWENYE RADIO ZA DAR” – AFANDE SELE…!!
09 July 2012

Posted on 09 July 2012

MSANII wa muzki wa Hip Hop kutoka pande za Morogoro Seleman Msindi ‘Afande Sele’, amesema kuwa haoni sababu ya kuleta nyimbo zake jijini Dar kwani haonekani kama ana umuhimu kutokana na radio nyingi kuzidharau nyimbo zake.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, msanii huyo alidai kwa sasa amekata tamaa ya kuleta kazi zake kwenye redio za Dar kwani hakunawanachokifanya zaidi kuziweka kapuni huku wakipiga za wasanii wa Dar pekee.

Hata hivyo alidai kuwa redio za dar zinaubanguzi wa mikoa kwani wasanii wengi wa wanotokea mkoani morogoro kazi zao hazipigwi kwa madai kuwa ni kutoka mikoani.

“Hakuna kipya Dar kwani nyimbo zetu kutoka morogoro hazipigwi na hii inatokana na kutubagua kwa madai kuwa ni wasanii wa kutoka mkoani lakini tunachotaka kusema ni kwamba bado muziki upo na uwezo tunao.” alisema Afande.

Aliongeza kuwa kama mashabiki wake wanahitaji kuona na kusikilzia kazi zake basi wazitafute kwenye mtandao kwani ndiko anapata mashabiki wengi kwa sasa.

Tags
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!