Posted on 09 July 2012
BAADA ya kufanya vizuri na ngoma yake ya ‘Nidangaye’ msanii Shetta, amesema kuwa kwa sasa yupo kwenye mchakato mpya wa kufanya
ngoma na mwanadada Lady Jay Dee, lakini bado wanabishana juu ya kuipa jina ngoma hiyo.
Akizungumza na DarTalk, Shetta alidai kuwa mbali na kubishana juu ya jina la ngoma yake kwa upande wake anaamini itaitwa ‘Bonge la Bwana’, ingawa hajataka kueleza maana halisi ya neno na maneno yatakayotumika.
Msanii huyo alisema kuwa kitendo cha kufanya ngoma na Lady Jay Dee ni kutokana na kumkubali mwanadada huyo nguli wa muziki tanzania kwani ana imani ngoma hiyo itakua nzuri kutokana na sauti yake.
“Baada ya ngoma yangu ya ‘Nidanganye Danganye’ kufanya vizuri kwa sasa nipo na Lady Jay Dee nataka kufanya naye ngoma ambayo najua itafanya vizuri hivyo mashabiki wangu naomba wakae mkao wa kula,” alisema Shetta.
Mambo vipi m2 mzima, mimi ni bongo la shabiki wako kwani nazikubali sana kazi zako uko juu mazazi kwa makamuzi hayo usirudi nyuma endelea kulisongesha gurudumu la bongo frever, kandamiza mwana mpaka mwisho umetisha mbayaaaa, Tunaisubili hiyo kazi utakayomshilikisha mwanadada mkari wa voko. BIG UP MEN.