
Posted on 09 July 2012
MSANII anayefanya muziki wa bongo fleva Felly Kano ‘Felly’, ameiambia DarTalk kuwa amekamilisha video ya wimbo wake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Hangover’, ambayo inatarajia kutoka hivi karibuni.
Akizungumza na mtandao huu msanii huyo mwenye maskani ya Oysterbay jijini Dar, alisema kuwa video hiyo imekamilika wiki iliyopita na sasa wanaendelea na editing ili iweze kuwa bomba zaidi.
Hata hivyo aliongeza kuwa audio yake inaendelea kufanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya redio, huku akiamini kuwa ujio wa kideo chake mambo si mabaya kwani mashabiki watapata kuona kila kitu nkinachozungumzwa ndani ya ngoma hiyo.
“Nilikuwa nimetoa audio peke yake hivyo baadhi ya rafiki zangu ambao nafanya nao kazi wakanishauri nitengeneze video na ndo imekamilika wiki iliyolipa na sasa kitu kinaendelea kutengenezwa hivyo mashabiki wangu wakae mkao wa kupokea kazi hiyo,” aliongeza.
Pamoja na yote Felly alidai kuwa mwaka huu anahitaji kutoa ngoma baada ya ngoma, pamoja kufanya zile za kimataifa ambazo ndizo kusudio lake kubwa katika muziki.