QUICK RACKA NA SHAA NDANI YA NGOMA ‘KATIKA’…!!
11 July 2012

Posted on 11 July 2012

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Quick Racka, amesema kuwa anatarajia kutoa ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Katika’, akimshirikisha mwanadada Shaa .

Akiongea na DarTalk, msanii huyo alidai kuwa kwa upande wake amesharekodi hivyo anayesubili ni mwanadada huyo ili naye atupie mistari yake ili kazi iweze kukamilika na kwenda sokoni.

Alisema kuwa ngoma hiyo itakuwa ni mfano wa club kwani katika video yake itaonesha amekutana na mtoto mrembo ambaye atakuwa anamuambia akatike ili aweze kuona utamu wake wa kucheza.

“Hi ni ngoma ambayo itaonesha nipo club hivyo nitakutana na mtoto mrembo ambaye nitakuwa nambembeleza akatike na ndiyo maana kubwa ya wimbo huu, na kikubwa nawaomba mashabikiz angu wausubili kwa hamu kwani ni bonge la pini,” aliongeza

Tags ,
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!