Posted on 12 July 2012
SIKU chache baada ya mtandao huo kuripoti kuwa video mpya ya msanii wa mziki wa kizazi kipya Ben Pol, ‘Maneno’, inatarajia kuigia sokoni hivi karibuni, sasa msanii huyo amesema kuwa tayari kazi hiyo imekamilika na leo itaanza kuonekana kwenye vituo mbalimbali vya televisheni.
Akiongea na DarTalk kwa mara nyingine tena msanii huyo alisema kuwa amesikiliza maoni ya mashabiki wake pamoja na familia yake hivyo ameamua kuipeleka haraka kazi hiyo ili wadau wake waweze kuiona.
“Nakumbuka siku chache nilizungumza hapa hapa DarTalk, na nikasema kuwa ngoma inatarajia kukamilika hivi soon, lakini leo naweza kusema kuwa kazi iko tayari na imeanza kusambazwa hivyo mashabiki wangu wataanza kuicheki kupitia televisheni,” alisema.
Mambo vp hii video imetulia ilembaya dah!mzazi wewe umejipanga xna big up