
Posted on 13 July 2012
MSANII wa filamu za kibongo Mariam Ismail, amesema kuwa baada ya kushirikishwa katika filamu kadhaa na kuonesha uwezo wa hali ya juu sasa anatarajia kuitoa kazi mpya inayokwenda kwa jina la ‘Apple’, ambayo itakuwa na nyota wengine kibao.
Akizungumza na mtandao huo msanii huyo alisema kuwa baadhi ya wasanii watakaocheza ndani ya filamu hiyo ni pamoja Baba Haji, Irene Uwoya ambaye ndiye muandaaji wa filamu hiyo na wengine kibao.
Alisema filamu hiyo inahusu mambo mbalimbali ya uchunguzi wa makosa jinai na mengine ya kusisimua ambayo yote yamekuwa yakitokea katika jamii yetu.
“Naweza kusema filamu hii itakuwa na matukio mengi lakini yote hayo yatahusu mambo ya uchunguzi kutokana na makosa mbalimbali yatakayokuwa yanafanywa na wahusika au kwa lugha rahisi itahusika sana na upelelezi,” alisema.