
Posted on 14 July 2012
WAKATI wadau mbalimbali wa tasnia ya filamu na hii ya bongo fleva wakilalamikia vijana wengi kukimbia shule na kuingia kwenye tasnia hizo, msanii Christine John ’Sintah’, amesema kuwa angekuwa na uwezo yenye kama yenye angeruhusu watu kuigia katika tasnia hiyo ni wale wenye elimu ya chuo kikuu, au chuo cha sanaa kwani tasnia hizo hazichukuliwi kama kazi nyingine zinazohitaji elimu.
Sintah alidai kuwa tasnia hizo zimekuwa kimbilio la vijana wasiyotaka shule ambao wanaamini kuwa kuingia huku kunaweza kuwatoa katika maisha, huku wakisahau kuwa wanahitaji na elimu ili waweze kufanya kazi katika kiwango cha kimataifa.
Hata hivyo msanii huyo aliongeza kuwa hata kwa wale warembo wanaotokea katika mashindano mbalimbali ya ulimbwende wanatakiwa kuheshimu tasnia hizo kwani, wasichukulia kama karata kuwa wanaweza kucheza kwani nao wanahitaji elimu ya kazi hiyo.
“Tanzania tunafanya mambo kwa sababu mtu fulani anafanya, kama tasnia hizi Filamu, Muziki, mitindo na nyingine, zinataratibu zake lakini hapa kwetu watu wanafanya kwa sababu kaka ni msanii au wengine baba alikuwa msanii lakini hatuna elimu ya hivi vitu na ndiyo maana hatuwezi kwenda mbele na kuonesha ubunifu wetu,” alidai.
Kwa upande wake alidai kuwa mwaka huu anaweza kwenda nje kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali juu ya filamu kwani anaamini endapo akifanya hivyo anaweza kutumia ujuzi huo kuwafundisha hata wengine.