MZEE CHILO AITABILIA MAKUBWA TASNIA YA FILAMU TANZANIA…!!
16 July 2012

Posted on 16 July 2012

NI wazee wachache wanaotamba katika tasnia ya filamu ndani ya Bara la Afrika, ambapo Mzee Chilo, ni miongoni mwao, ambapo amesema kuwa anaamini tasnia hiyo baada ya miaka 5 mbele itakuwa ghali sana kwani kadri siku na miaka inavyokimbia ndivyo thamani ya tasnia hiyo inavyoongezeka huku wasanii wake wakizidi kupata heshima kubwa.

Mzee Chilo anaamini kuwa tasnia hiyo itakafikia kipindi itakuwa ghali kwani hata vijana watakaotaka kuigia na kufanya kazi hiyo watakakuwa na wakati mgumu wa kuweza kuigia kwani kuna uwezekano mkubwa kukawa na vikwazo pamoja na sheria ya kuzuia utitilii wa wasanii.

Msanii alisema kuwa hakuna kinachoweza kuifanya tasnia hiyo kushindwa kuwa juu baada ya miaka hiyo kwani ilikotoka haikuwa na umaarufu kama ilivyo sasa kwani hata wasanii waliopo wanatumia nguvu na uwezo wao kwa lengo la kuipeleka mbele tasnia hii.

Aliongeza kuwa ingawa wapo baadhi ya wasanii wanaofanya kazi hiyo kwa maslahi yao pekee na pasipo kujali uwakilishi wa nchi kimataifa lakini bado kuna uwezekano mkubwa wa kujulikana zaidi na kufikia ama kuzidi level za wasanii wa Nigeria au Ghana ambao wako juu kwa sasa upande wa Africa.

Tags
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

One Response

  1. YUSUPH MAZIGE says:

    na amini kuwa tasinia ya filamu itafika mbali endapo wasanii wata acha majungu so inabidi muji epushe na majungu ok


LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!