
Posted on 20 July 2012
BAADA ya kulejea nchi juzi wakitokea nchini Italy walikoenda kufanya shoo, Bendi ya muziki wa Taarabu Mashauzi Classic. imesema kuwa imejifunza mambo mengi kutoka kwa watu wa kule ikiwemo namna ya kufanya shoo laivu za jukwaani ambazo huleta mvuto kwa watazamaji.
Akizungumza na DarTalk mmiliki wa bendi hiyo Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’, au unaweza kumuita Simba Dume, Alisema bendi yake ilipata mualiko huo baada ya kuonekana inafanya vizuri hapa Tanzania.
Alisema kuwa wamekaa huko kwa takribani mwezi mmoja lakini kikubwa wamejionea ni namna gani watu wanavyopenda muziki wa taarabu kwani wamefanya shoo miji mikubwa ya nchini humo na watu wengi walikuwa wanajitokeza kutazama.

Mashauzi Classic kazini
“Safari yangu naweza kusema imekuwa na mafanikio makubwa kwani watu wengi walikuwa wanakuja kutazama tunafanya nini na kila sehemu ambayo tunapiga shoo watu walikuwa wanafurika kwa wingi na hii inaonesha wazi kuwa muziki huu unapendwa duniani kote,” alisema.
Hata hivyo aliongeza kuwa mbali na muziki wao kupendwa zaidi lakini wanaamini makamuzi waliyoyafanya huko yamewapa funzo tosha kwani kwa sasa watakuwa wameiva kiasi kwamba hakuna bendi nyingine yoyote itakayo wasumbua kichwa.