WASANII WALIOTAMBA NA TAMTHILIA YA ‘JUMBA LA DHAHABU’ WAKUTANISHWA TENA…!!
20 July 2012

Posted on 20 July 2012

WASANII kibao waliowahi kutamba na tamthilia ya ‘Jumba La Dhahabu’, ambao kwa sasa ndiyo wanafunika ndani ya bongo movie, wameungana tena pamoja baada ya mrefu kutoonekana kwenye kazi ya pamoja kutokana na kila mmoja kufanya filamu kivyake baada ya mafanikio waliyoyapata.

Akizungumza na DarTalk mkurungezi wa kampuni ya Tuesday Entertainment inayojihushisha na utengenezaji wa filamu na tamthilia Tuesday Kihangala ‘Mr Chuzi’, alisema kuwa wasanii hao wameamua kurudisha nguvu zao pamoja ili waweze kutengeneza kazi zitakazoteka zaidi soko la tamthilia pamoja na filamu.

Alisema kwa upande wake kuungana tena kwa wasanii hao anaona ni mwazo mzuri kwani anaamini sasa kila mmoja amekwiva hivyo wataweza kufanya mambo makubwa zaidi ambayo hayatakuwa na mfano.

“Wasanii wote waliyotamba na kuipa heshima tamthilia ya ‘Jumba la Dhahabu’, sasa wameungana tena na tupo pamoja, naweza kusema huu ni mwazo mzuri kwa sababu nguvu ya watu wengi ndiyo inayoweza kutengeneza kitu kuzuri,” alisema.

Baadhi ya wasanii waliotamba katika ‘Jumba la Dhahabu’ ni Mzee Chilo, Jini Kabula, Jack wa Chuz, Kojack na wengine kibao ambao tukiwataja kwa majina hayuwezi kuwamaliza.

Tags
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!