“NIMEFUNGA MWEZI MTUKUFU LAKINI NAENDELEA KUFANYA MUZIKI KAMA KAWA” – ISHA MASHAUZI…!!
22 July 2012

Posted on 22 July 2012

MSANII anayefanya vizuri kwenye muziki wa taarabu nchini Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’, amesema kuwa amefunga kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani lakini haimanishi kwamba amefunga na shunguli zake za muziki kwani hizo ndizo zinazompa kula mjini na kuendesha familia.

Akiongea na DarTalk msanii huyo alisema kuwa muziki kwake ni kazi hivyo endapo akisimama mwezi mzima anaweza kufa njaa, hivyo anaendelea na muziki na hata akipata show kipindi hiki anafanya kwa lengo la kutoa burudani kwa mashabiki wake.

Alidai kuwa kikubwa atatumia kipindi cha mwezi mtukufu kuangalia safu yake ya uimbaji ili kuweza kuiweka katika kiwango kizuri zaidi.

“Mwezi mtukufu haimanishi kwamba hata muziki pia watu wanafunga hapana kikubwa ni kumuomba mungu na kutubu makosa yetu kwani, hiki ni kipindi kizuri cha kutafakali kila hatua ambayo tumepitia,” alisema Isha

Tags
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

2 Comments

  1. JOSEPHINE MGAYA says:

    KUFUNGA RAMADRANI HAIMAANISH KUACHA SHUGHULI ZA KUKUINGIZIA KIPATO ILI MAADILI HAIMCHUKIZI MUNGU HATA MUNGU ALISEMA ASITEFANYA KAZI NA ASILE KAMUA ISHA UPO JUUUUU

  2. kunte says:

    huna funga vutu we


LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!