“NAMCHUKULIA ‘NEY WAMITEGO’ KAMA KAKA AU RAFIKI NA SI VINGINE”- NISHA…!!
26 July 2012

Posted on 26 July 2012

BAADA ya msanii wa muziki wa kizazi kipya Ney Wa Mitego, kulalamika na kutangaza kuwa anampenda mwanadada wa kwenye tasnia ya filamu bongo Salma Jabu ‘Nisha’, hali imekuwa tofauti na vile alivyotarajia kwani kimwana huyo ameamua kuweka wazi kuwa hamchukii ‘Ney’ lakini anamchukulia kama kaka au rafiki.

Ney wiki chache zilizopita aliongea sana kwenye vyombo vya habari, na kudai kuwa mapenzi yake kwa Nisha, ni zaidi ya mapenzi lakini alikuja kuumia moyo baada ya kuambiwa kuwa mwanadada huyo amemtambulisha mchumba ake, wakati yenye amekolea kitambo kwa mrembo huyo.

Baada ya utambulisho huo kufanyika ‘Ney’, alitoa kauli kuwa hata kama amenyimwa mapenzi na mrembo huyo wa bongo muvi lakini anaamini Mungu atamlipa kwa hali yoyote, na hakuishia hapo ambapo aliamua kuonesha mapenzi yake kwenye mtandao wa Facebook kwa kuweka picha ya ‘Nisha’ ili kila mtu aweze kujua.

Baada ya harakati hizo na misukosuko kibao, mwanadada Nisha aliamua kufunguka zaidi na kusema kuwa anamchukulia Ney Wamitego kama rafiki yake pengine kama kaka hivyo anashindwa kuelewa ni kitu gani kinachomsumbua Ney juu yake.

“Mimi nilimtambulisha mpenzi wangu na Ney aliposikia ishu hiyo akaanza kuongea kwenye vyombo vya habari kuwa ananipenda, lakini ninachoweza kusema ni kwamba namchukulia kama kaka, kwani siwezi kuwana wapenzi wawili kwa wakati mmoja,” aliongeza.

Nisha aliongeza kuwa mwezi huu ni mtukufu hivyo haitaji kusema uongo hivyo ameamua kuweka wazi ishu hiyo ili hata mashabiki wake waweze kujua, ishu nzima ilivyokuwa kutoka kwa Ney, lakini anaamini kuwa hawana chuki.

Tags
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!