“AUNTY EZEKIEL” KUFUNGA NDOA OCTOBER, PIA KUFUNGA MWAKA NA FILAMU MBILI…!!
30 July 2012

Posted on 30 July 2012

ILE kasumba kwamba hakuna msanii wa bongo muvi anayeweza kuolewa na kudumu ndani ya ndoa, inatarajia kufutwa na msanii Aunty Ezekiel, ambaye anatarajia kufunga ndoa mwezi October mwaka huu, na mpenzi wake anayeishi Dubai ambako ndiko atakoenda kuishi baada ya kufunga ndoa.

Mtandao wa DarTalk, ulifanya mazungumzo mafupi na msanii huyo juu ya maisha yake na filamu kwa ujumla ambapo, alisema kuwa ameamua kuchukua maamuzi hayo ya kutaka kufunga ndoa kwani anahitaji kuishi na mtu ambaye wataweza kupanga naye maisha.

Alidai kuwa mpenzi wake huyo ni Mtanzania ingawa anaishi nje, ambapo anaamini baada ya kufunga ndoa na yeye anataweza kwenda kufanya kazi huko.

“Nilikuwa kimya juu ishu hii lakini nachotaka kusema ni kwamba mambo yangu sasa yameanza na nimeamua kufunga ndoa, hivyo mashabiki wangu nahitaji nao waweze kujua kuwa sasa nimeamua kuchukua maamuzi hayo,” alisema.

Ezekiel alisema kuwa vikao vya harusi na kupanga itakavyokuwa wameshaaza kukaa, kwani wameanza Jumapili.

Aliongeza kuwa mbali na mchakato huo mkubwa pia mwaka huu wa 2012 kampuni yake inatarajia kufunga mwaka kwa kutoa filamu mbili ambazo anaamini zitakuwa moto wa kuotea mbali.

Tags ,
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

2 Comments

  1. Frankiekyse says:

    Huyu b dada mi namkubali sanaaaaaaaaa.1 anapenda kuji2ma.2 hana habari na m2.mi nampa big up ileèéèë mbayaäåàáâ

  2. Bayuu Yuu says:

    Hawa jamaa waandishi wazushi tu ndoa haina utata wala bwamdogo hatafutwi na polisi mimi ni kaka yake huyo mume Wa Aunty Ezekiel naishi Switzerland mukitaka ukweli wasilianeni na mimi na mwisho juzi tu niliongea nao wote wawili na Aunty bado yupo Dubai anapoishi mumewe na wala sio India kama inavyozushwa ktk magazeti habari ndo hiyo


LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!