
Posted on 30 July 2012
WASANII chipukizi wanaofanya vyema kwenye tasnia ya filamu bongo, Mariam Ismail na Esther Flavian, bifu lao limezidi kukua huku likiwa kubwa zaidi ambapo wote kwa pamoja wanadai kuwa hakuna anayetaka kukaa meza moja na mwenzake na kulitafutia ufumbuzi bifu lao lililodumu kwa takribani miaka miwili sasa.
Wasanii hao walikuwa wakifanya kazi pamoja lakini walikuja kutofautiana baada ya mmoja wao kuonekana akifanya vizuri katika filamu kadhaa huku mwingine akiwa hana nafasi katika hizo filamu.
Mwandishi wa DarTalk aliwatafuta wasanii hao ili kujua wamefikia wapi juu ya kutafuta ufumbuzi wa ishu hiyo, ambapo walidai kuwa hakuna anayetaka kukaa mezani na wataendelea kuwa Simba na Chui.
Mariam alidai kwa upande wake hana muda wa kukaa na muhuni ambaye anawivi wa maendeleo kwani anaamini Esther hakuna anachokiwaza zaidi ya umaskini.
“Mimi nafanya filamu tena na wasanii wakubwa na hicho ndicho kinachomuumiza huyo mdada, hivyo sina muda wa kukaa naye chini kwa sababu hakuna anachowera kuniambia,” alidai Mariam.
Wakati huo huo Esther naye aliongeza kuwa hawezi kukutana na mwanamke anayependa kufuata mkumbo kwani, “Mariam hana chochote zaidi ya kusubili kupewa nafasi za bure katika filamu,” alidai Esther.