“LINAH” AONGELEA UJIO WA NGOMA MPYA, GARI YAKE AINA YA BMW NA UPCOMING UK TRIP…!!
08 August 2012

Posted on 08 August 2012

MSANII anayefanya vizuri kwenye soko la muziki wa kizazi kipya kwa upande wa wanawake Linah Sanga ‘Linah’, a.k.a Ndege Mnana ameumbia mtandao wa DarTalk, kuwa baada ya kutoka Marekani alikoenda kikazi sasa anatarajia kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Ushafahamu’, ambayo itaigia sokoni siku chache zinazokuja.

Akilonga na mwandishi wa DarTalk, Linah, alisema kuwa ngoma hiyo itakuwa ni ya kwanza kutoa tangu aliporudi kutoka nje hivyo anaamini itafanya vizuri kwani maandalizi na uwezo wake katika kazi hiyo ni mkubwa mno.



Linah akiwa na mashabiki wake kwenye moja ya show alizofanya USA

Alisema kuwa ikiwa sokoni ngoma hiyo atakuwa katika mchakato wa video , ili mashabiki wake wapate burudani zaidi kutoka kwake.

“Hiyo ni ngoma ambayo nimeifanya mwenyewe baada ya kutoka Marekani, lakini ipo nyingine pia ambayo nimefanya na Amini, ambayo hata hivyo jina la ngoma hiyo nahisi itaitwa ‘Linah na Amini’, kwa sababu tumefanya si tu kwa kushirikishishana bali kwa ushirikiano,” alisema.

Hata hivyo mwadada Linah aliongeza kuwa anatarajia kusafiri kikazi kwenda UK ambapo atakuwa huko kanzia Agosti 23-24.

Sambamba na michakato hiyo hakusita kueleza kuwa katika kujiimalisha kimaisha tayari amesha nunua mkoko mpya aina ya BMW ambao mashabiki watapata nafasi kuuona hapa hapa DarTalk akisha maliza taratibu zote. Keep it locked!

Tags
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!