“ALBAMU YA ‘SHIKA HAPA ACHA HAPA’ KUINGIA SOKONI MWEZI NOVEMBA MWAKA HUU” – H-BABA…!!
18 September 2012

Posted on 18 September 2012

WAKATI wasanii wengine wakitupilia mbali mawazo ya kutoa albamu kwa madai kuwa hazina soko na wanaibiwa sana msanii anayetesa na ngoma yake ya ‘Thamani Yetu’H-Baba, amesema kuwa anatarajia kuachia albamu yake Novemba mwaka huku ikiwa imepewa jina la ‘Shika Hapa Acha Hapa’, itakayokuwa na nyimbo 10.

H-Baba alizitaja baadhi ya nyimbo zitakazokuwa ndani ya albamu hiyo kuwa ni pamoja na ”Thamani Yetu, ‘Shika Kichwa’, ‘Huendani Nami’, ‘Nipe Kidogo’, ‘Shika Hapa Hacha Hapa’ na nyingine kibao ambazo hajawahi kuziachia.

Alisema kuwa kwa upande hataki kusikiliza maneno ya watu kuwa albamu hazifanyi vizuri skoni kwani kila mtu anafanya anachojua na hakuna msanii anayetangaza kuwa albamu yake haijafanya vizuri.

“Wasanii wengi wanalalamika kuwa albamu hazifanyi vizuri nachoweza kusema ni kwamba kulalamika kwa mtu fulani hakuwezi kiunifanya mimi nishindwe kufanya kazi zangu za kila siku, albamu nitatoa na naamini mashabiki wataipokea na itafanya vizuri,” alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa baada ya ngoma yake hiyo ya ‘Thamani Yetu’, ambayo inafanya vizuri kwenye vituo vingi vya televisheni soon atakuja na kitu alichomshirikisha msanii wa muziki wa dansi Banza Stone ambaye hivi sasa yupo katika bendi ya Extra Bongo.

Tags
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!