‘AUNTY EZEKIEL’ AFUNGUKA….AMTAKA ‘NISHA’ AACHE KUJISHAUA…!!
19 September 2012

Posted on 19 September 2012

BAADA ya msanii wa filamu Salma Jabu ‘Nisha’, kulitaka Baraza la Sanaa la Taifa ’BASATA’, kumchukulia hatua kali msanii Aunty Ezekiel kwa madai picha zake za nusu utupu zinachafua maadili na kuwafanya wasanii wote waonekane wahuni, naye amekuja juu na kumtaka Nisha afanye mambo yake na aache tabia ya kumfuatilia.

Hata hivyo baada ya kutokea ishu ya Ezekiel bado wasanii wanaendelea kukumbwa na skendo chafu kwani naye Wema Sepetu kuna baadhi ya picha mitandaoni zinamuonesha sehemu kubwa makalio yake yakiwa wazi kitu ambacho kinaendelea kuwamaliza bongo movie.

Ezekiel alidai kuwa haoni sababu ya Nisha, kumtolea maneno hayo kwani hata yeye ana matatizo yake hivyo anatakiwa kujichunguza yeye ndipo aende kwa mtu mwingine.

Alidai kwa sasa anatumia lugha ya kistaarabu zaidi yani haitaji bifu lakini akizidi kumfuatilia atachanua makucha, ingawa hana tabia ya kuchukuiana na mtu ila kwa hili hajakubaliana nalo kwani wapo wasanii wagapi wanakosea na hajawahi kutoa kauli kama hiyo.

Hata hivyo aliongeza kuwa asitake kutumia kauli za mpenzi wake Ney, kuwa makahaba wako bongo movie kwani hata mwenyewe ni mmoja wa wasanii wa tasnia hiyo.

Tags ,
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

2 Comments

  1. Paul mrimi says:

    We aunt acha uwambiwe ukweli; kwani zile picha zinaishushia hadi bongo movie.Unapiga picha za uchi kisha unasingizia pombe! kwan pindi unavaa hizo nguo ulikuwa umelewa?

  2. adelqueen james says:

    bongo movie mnachekesha shame on u all


LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!