‘BANANA ZORRO’ MBIONI KUACHIA AUDIO NA VIDEO YA NGOMA YAKE YA ‘SIJAONA’…!!
19 September 2012

Posted on 19 September 2012

MKONGWE ndani ya muziki wa bongo fleva Banana Zorro, ameuambia mtandao wa DarTalk, kuwa siku chache zijazo ataachia audio na video ya ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Sijaona’, ambayo amefanya na msanii mahiri wa miondoka ya R&B Nurueli.

Banana alisema kuwa ngoma hiyo inahusiana na mahaba hivyo anaamini itakuwa suluhisho tosha kwa watanzania ambao siku zote wamekuwa wakiumizwa na mapenzi hasa na mashabiki wake ambao ndiyo walengwa wakubwa wa kazi zake.

Alisema ameamua kufanya collabo na msanii Nurueli katika kibao chake kwani anaamini kipaji chake na uwezo wake wa kuimba ni mkubwa na unaweza kukipa chati kubwa kibao chake hicho.

“Katika ngoma yangu hii nimeamua kumpa shavu ndugu yangu huyo kwa sababu najua kiwango chake, hivyo nawasihi mashabiki wangu ikitoka ngoma hii waone na watoe mawazo yao,” alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa baada ya kazi hii kwenda sokoni atakuwa katika harakati za kutengeneza ngoma nyingine ingawa hadi sasa bado hajaipa jina lakini atafanya na wasanii wawili ambao ni Barnaba na Amini.

Tags ,
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!