‘LATIPHER MKUU’, SILAHA NYINGINE NDANI YA ‘WORLD OF BENEFIT’…!!
10 March 2013

Posted on 10 March 2013

Jina lake halisi ni Latipher Mkuu, si maarufu sana machoni pa watu lakini ni mahiri sana katika kazi, kama ulivyo mvuto wa umbile lake ndivyo alivyo na mvuto katika kazi ya sanaa ya uigizaji. Kipaji chake kimedhihirika hivi karibuni baada ya kupata fursa ya kushiriki katika filamu yaWorld Of Benefit’ ambayo ipo katika hatua ya editing ikisubiri kuingizwa sokoni.

Licha ya ushiriki wake wa scene chache ndani ya filamu hiyo lakini Latipher ameweza kuonesha kipaji cha hali ya juu akiwa sambamaba na mkongwe Rose Ndauka.



Latipher katika pozi

Akizungumzia umakini wake katika kazi Latipher amesema hivi, “Awali, sikuwa na uzoefu mkubwa katika mambo ya uigizaji, lakini baada ya kukaa kambini kwa siku kadhaa na kupata mafunzo ya kutosha kutoka kwa wasanii wakongwe nilijikuta nikiingiwa na ujasiri, papo hapo nilianza kujituma na kufanya mazoezi bila kuchoka, nafurahi kuona nilichokipigania kimefanikiwa, nitaendelea kujifunza zaidi ya hapa ili baadae niwe muigizaji bora kabisa wa filamu.”

Washiriki wengine aliokutana nao Latipher katika filamu hiyo ni pampja na Mzee Chilo, Hemed Suleiman, Awadh Saleh, Mama Mjata, Timbulo, Peter, Tutti, Miriam na Natalia.

Tags ,
< PREVIOUS POST
NEXT POST >
Most Read News

4 Comments

  1. JULIANA says:

    TUNAISUBIRI WORLD OF BENEFIT, inatoka lini?

  2. Jerry says:

    Namkubali sana Rose Ndauka

  3. GEORGE says:

    Hakika unavutia sana na pia hiyo filamu yako nahisi itakuwa funika bovu,maana huo mvuto ni nooomaaaaaaaaa!

  4. mubbah kengs says:

    So xcitng……len me Waitn for dc


LEAVE A COMMENT

NOTE: To comment it is better that you have a gravatar account.
You can get a free gravatar account by clicking here.








SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!